Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi 6 Nyama ya ng'ombe (nusu kilo) Viazi mviringo 2 Kitunguu swaum Tangawizi Kitunguu maji Nyanya 1 kubwa Mafuta (vegetable oil) Chumvi Limao Pilipili
Matayarisho
Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama nyeupe na nyama nyekundu.
Nyama nyeupe
Hizi ni nyama zitokanazo na samaki, kuku, ndege wa aina zote, bata, wadudu
Nyama nyekundu
Hutokana na ngβombe, mbuzi, kondoo,nguruwe na wanyama wa porini.
Nyama ina virutubishi vingi muhimu kwa afya ya binadamu kama protini, vitamini na madini. Madini ya chuma yanayopatikana kwenye nyama ni rahisi sana kusharabiwa (kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwa kuongeza wekundu wa damu. Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuyeyusha chakula na kusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua. Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingi unaweza kuwaletea matatizo hasa katika uyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundu si rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyama nyeupe.
Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengi wanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana na mara chache. Si vyema watu hawa waache kabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu ni kutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hii iyeyushwe kwa urahisi tumboni.
Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamoja n a : -
β’ Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya kusaga (kwa wanaoipata). β’ Kupika nyama na viungo vinavyosaidia kulainisha kama vile papai bichi, limao, vitunguu saumu n.k. β’ Kula nyama pamoja na papai
Kwa hiyo, kwa anayepata nyama nyekundu kwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyo na kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwa yule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyama nyekundu asiache kutumia kwani ina umuhimu mwilini mwake.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi
Mchele wa basmati - 3 vikombe
Kuku - Β½
Bilingani - 2 ya kiasi
Viazi - 4
Vitunguu - 2
Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 2
Chumvi - kiasi
Garama masala (mchanganyiko wa bizari) - 1 kijiko cha chai
Hiliki ya unga - ΒΌ kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia wali - ΒΌ kikombe
Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele. Kata kuku vipande upendavyo safisha Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala). Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria. Menya na kata viazi kaanga weka kando. Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo. Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa. Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive. Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ulezi (millet flour vijiko 3 vya chakula) Maziwa fresh (milk 1/2 kikombe) Sukari (sugar 1/4 ya kikombe cha chai) Siagi (butter kijiko 1 cha chakula) Maji (vikombe 4 vya chai) (serving ya watu wawili)
Matayarisho
Chemsha maji ya uji, Kisha koroga unga na maji ya baridi kiasi na uchanganye kwenye maji ya moto yanayochemka. Endelea kukoroga mpaka uchemke ili kuhakikisha uji haupatwi na madonge. Ukishachemka tia, maziwa, sukari na butter. Kisha acha uchemke kwa muda wa dakika 10 na hapo uji utakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Tende zilizotolewa kokwa - 1 Kilo
Cornflakes - 1 Β½ kikombe
Lozi Zilokatwa katwa - 1 kikombe
Siagi - ΒΌ kilo
MANDALIZI
Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10. Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri. Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri. Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo. Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).
Mahitaji
Kuku mzima Nyanya kubwa 3 Karoti mbili Pilipili hoho Kotmiri Tangawizi Kitunguu maji Kitunguu saumu kidogo Ndimu Mafuta ya kupikia Chumvi (pilipili ukipenda)
Matayarisho
1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja. 2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu). 3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni. 4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni. 5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni. 6. Andaa kikaango na jiko.
Mapishi
1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui). 2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi. 3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana. 4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako. 5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu. Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 3 Vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Mayai 3
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini. Tia unga na baking powder changanya na mwiko. Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi. Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma. Pika (bake) katika oven moto wa 350Β°F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Safisha samaki kisha mmarinate na tangawizi, kitunguu swaum, chumvi na limao kwa muda wa masaa mawili. Baada ya hapo menya viazi na uvikate vipande vidogo kisha vioshe na viweke kwenye sufuria yenye maji kiasi kwa ajili ya kuvichemsha. Viinjike jikoni na uviache vichemke kwa dakika 7. Vikisha chemka tia samaki, katia kitunguu,pilipili, chumvi, limao, vegetable oil na nyanya na uache supu ichemke mpaka samaki na viazi vitakapoiva. baada ya hapo supu itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele 2 vikombe vya chai Choroko kikombe 1 na 1/2 Nazi kopo 1 Swaum 1 kijiko cha chakula Kitunguu 1 kikubwa Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai Chumvi Mafuta
Matayarisho
Loweka choroko usiku mzima, pindi ukianza kupika loweka mchele nusu saa kisha katika sufuria kubwa, kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia swaum na binzari nyembamba kisha tia choroko, mchele, chumvi,nazi na maji mengi kiasi yakuivisha choroko pamoja na mchele. Pika mpaka vitu vyote viive na viwe vilaini kisha upondeponde kiasi.Baada ya mseto wako kuiva utakuwa unaonekana kama uji wa mchele vile. Na Baada ya hapo mseto wako utakuwa tayari kwa kuliwa na mboga yoyote uipendayo.Inapendeza zaidi kuliwa vile tu ukishamalizwa kupikwa