Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi Vya Masala
Nyama vipande - 3 LB
Mtindi - Β½ kopo
Kitunguu (thomu/galic) - 1Β½ kijiko cha supu
Tangawizi - 1Β½ kijiko cha supu
Nyanya - 2
Pilipili mbichi - kiasi
Nyanya kopo - 4 vijiko vya supu
Vidonge supu - 2
Pilipili nyekundu paprika - kiasi
Bizari zote saga - 2 vijiko vya supu
Viazi - 4
Mafuta - 2 mug
Samli - Β½ kikombe
Vitungu - 6
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika masala
Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya vyote pamoja weka motoni. Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni. Kanga viazi weka pembeni. Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke. Tia viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama acha moto mdogo.
Vipimo Vya Wali
Mchele - 5 mug
Maji - kiasi
Chumvi - kiasi
Mafuta uliyokaanga vitungu - kiasi
Rangi ya biriani - ΒΌ kijiko cha chai
*Zafarani - Β½ kijiko cha chai
*roweka rangi na zafarani
Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali
Osha mchele roweka muda wa saa. Chemsha maji kama magi 10 hivi na chumvi tia mchele. Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja. Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika. Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mara nyingi biringanya hutumika kama kiungo cha nyongeza katika mchuzi. Hata hivyo, kiungo hiki kinaweza kupikwa chenyewe na kutoa mchuzi wenye ladha ya kipekee.
Baadhi ya wapishi wameweza kubuni aina hii ya upishi ambayo huweza kupikwa kwa dakika tano tu na kukupa chakula kitamu chenye ladha ya kuvutia.
Uzuri wa chakula hi ni kwamba kinaweza kuliwa wakati wowote na kwa chakula chochote kulingana na matakwa ya mlaji.
Kwa mujibu wa wataalamu wa maswala ya mapishi, biringanya ni miongoni mwa vyakula vyenye mapishi mengi kama ilivyo kwa mchele. Hapa tutaenda kuona jinsi ya kupika roast ya biringanya na mayai.
Mahitaji:
Biringanya 2 kubwa Nyanya 4 kubwa Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani Mayai 2 Mafuta ya mzeituni vijiko vitatu vya mezani Chumvi kiasi Pilipili 1 (kama unatumia) Hoho 1 Karoti 1 Kitunguu swaumu kilichosagwa 1 Kotimili fungu 1
Maadalizi:
Chukua biringanya ioshe vizuri na kasha katakata vipande vidogo vidogo. Osha na menya nyanya hapafu katakata. Fanya hivyo kw akaroti na hoho pia. Weka mafuta kwenye sufuria na weka jikoni kwenye moto kiasi Yakishachemka maji na kasha weka kitunguu maji na kasha swaumu huku ukikaanga taratibu. Weka hoho na karoti huku ukiendelea kukaanga. Baada ya hapo weka nyanya na baadae chumvi. Funika hadi ziive kabisa na kasha weka majani ya kotimili. Weka biringanya. Acha vichemke hadi viive. Koroga ili kuruhusu mchanganyiko wako uchanganyike vizuri. Kwa kuwa biringanya ina majimaji huhitaji kuweka maji ya ziada, weka pilipili. Acha kwa muda wa dakika tatu hadi dakika tano. Pasua mayai na kisha miminia huku ukikoroga taratibu. Fanya hivyo hadi yaive kabisa na kuwa mchuzi mzito. Roast yako ya biringanya iko tayari kwa kuliwa Unaweza kula aina hii ya mboga na mikate, maandazi na hata ugali
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Ndizi mbichi - 10
Nyama - kilo 1
Nazi ya kopo - 1
Chumvi - 1 Kijiko cha chakula
Ndimu - 1
Bizari ya manjano - 1 Kijiko cha chai
Pili pili mbichi - 3
Nyanya (tomatoes) - 2
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chakula
Namna ya Kutayarisha Na Kupika
Kata nyama vipande vipande na uisafishe. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda. Weka pembeni zipoe. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Tende zilizotolewa kokwa - 1 Kilo
Cornflakes - 1 Β½ kikombe
Lozi Zilokatwa katwa - 1 kikombe
Siagi - ΒΌ kilo
MANDALIZI
Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10. Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri. Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri. Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo. Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:44 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Njia za kupima Afya
Njia mbalimbali hutumika kupima hali ya lishe, njia hizi ni;
1. Vipimo vya umbile la mwili
2. Vipimo vya maabara
3. Kuchukua historia ya ulaji na maradhi
Vipimo vya umbile la mwili
Baadhi ya vipimo ambavyo vinaweza kutumika kutoa tahadhari kuhusu magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ni;
1. Uwiano wa uzito na urefu au Body Mass Index (BMI).
2. Mzunguko wa kiuno.
3. Uwiano wa mzunguko wa kiuno na nyonga.
4. Kulinganisha uzito na umri.
Uwiano wa uzito na urefu au Body Mass Index (BMI).
Hiki ni kipimo kinachotumika kuangalia uwiano wa urefu na uzito wa mtu, ni muhimu kuchukua vipimo kwa usahihi.Uwiano wa uzito katika Kilogramu na urefu katika mita hupatikana kwa kutumia kanuni ifuatayo:
BMI= uzito (Kg)/Urefu2 (m2)
BMI huwa na viwango mbalimbali vilivyowekwa na shirika la Afya duniani (WHO) kutafsiri hali ya lishe ya mtu ambavyo ni
1. BMI chini ya 18.5 = uzito pungufu.
2. BMI kati ya 18.5 mpaka 24.9= uzito unaofaa.
3. BMI kati ya 25.0 mpaka 29.9 = unene uliozidi.
4. BMI ya 30 au zaidi = unene uliokithiri au kiribatumbo.
Mahitaji ya chakula mwilini hutegemea umri, jinsi, hali ya kifiziolojia (kama ujauzito na kunyonyesha), hali ya kiafya, kazi na mtindo wa maisha. Uzito wa mwili hutegemea na chakula unachokula, pamoja na shughuli unazofanya, mara nyingi unene hutokana na kula chakula kwa wingi. Unene uliokithiri unachangia kwa kiwango kikubwa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo kubwa la damu, na saratani. Uzito uliozidi unapaswa kupunguzwa ili kuepuka magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza
Jinsi ya kupunguza unene uliozidi
1. Tumia mafuta kwa kiasi kidogo kwenye chakula
2. Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi hususani vinavyopikwa kwa kudumbukizwa kwenye mafuta, au vinavyokaangwa kwa mafuta mengi.
3. Epuka matumizi ya vinywaji au vyakula venye sukari nyingi
4. Epuka asusa zenye mafuta mengi au sukari nyingi kati ya mlo na mlo.
5. Ongeza vyakula venye makapi- mlo kwa wingi kama matunda, mboga mboga na nafaka zisizokobolewa.
BMI haitumiki kwa wanawake wajawazito, BMI haitumiki kwa watoto na vijana walio na umri chini ya miaka 18, BMI haitumiki kwa watu wasioweza kusimama vyema, waliovimba miguu, na wanawake wanaonyonyesha katika miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo Nyanya ya kopo 1/2 Kitunguu 1 Curry powder 1/2 kijiko cha chai Chumvi Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ngβombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:38 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Mchele wa pishori (basmati) - 4
Vitunguu katakata - 3
Nyanya (tungule) katakata vipande vikubwa - 3 -5
Pilipili boga la kijani (capsicum) katakata
Supu ya kitoweo au vidonge vya supu - 1
Bizari mchanganyiko Garama masala - 5-7
Pilipili mbichi ya kusaga - Kiasi
Zaafarani ya maji (flavor) - 1 kijiko cha chakula
Mafuta ya kupikia - ΒΌ kikombe
Samaki wa kukaanga
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Roweka mchele kiasi nusu saa kisha chemsha mchele kwa supu uive nusu kiini. Mwaga maji chuja. Wakati mchele unapikika, weka mafuta katika sufuria kubwa ya kupikia wali, kaanga vitunguu mpaka vigeuke rangi ya hudhurungi. Tia nyanya na vitu vinginevyo vyote kaanga kidogo tu. Mwaga wali katika sufuria na nyunyizia zaafarani kisha changanya na masala vizuri. Funika upike katika oven (bake) au juu ya stovu moto mdogo mdogo kiasi dakika 15- 20. Epua ikiwa tayari, pakua kwenye sahani kisha tolea kwa samaki wa kukaanga.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage yaliyochemshwa kiasi Spinach zilizokatwa kiasi Vitunguu maji 2 Nyanya 1/2 kopo Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry powder 1 kijiko cha chai Olive oil Chumvi
Matayarisho
Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.