Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:34:53 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Vikombe
Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu
Maziwa ΒΎ Kikombe
Iliki Kiasi
Mafuta ya kukarangia Kiasi
Shira
Sukari 1 Kikombe
Maji ΒΎ Kikombe
Vanila Β½ Kijiko cha chai
Zafarani (ukipenda) Kiasi
Jinsi ya kupika na kuandaa
Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa Basmati /Pishori - 4 vikombe
Kuku
Vitunguu - 3
Nyanya/Tungule - 2
Tangawizi mbichi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi nzima - 3
Ndimu - 2
Garama Masala/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
Haldi/tumeric/bizari manjano - 1 kijiko cha chai
Pilipilu ya unga nyekundu - 1 kijiko cha chai
Mtindi /yoghurt - 3 vijiko vya supu
Mafuta Β½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele, roweka. Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli. Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu. Punguza mchanganyiko kidogo weka kando. Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi. Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive. Epua, weka kando. Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando. Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali. Tia kuku uchaganye vizuri. Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja. Punguza masala nusu yake weka kando. Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali. Funika upike katika oveni hadi uive. Changanya unapopakua katika sahani.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Maziwa mazito matamu (condensed milk) - 2 vibati
Sukari - 1 kikombe
Samli 1 Β½ kikombe
Vanilla 2 kifuniko cha chupa yake
Hiliki ilosagwa - 2 vijiko vya chai
Sinia kubwa ya bati Paka samli
MAANDALIZI
Changanya maziwa, sukari na samli katika sufuria isiyogandisha chakula (non-stick) uweke katika moto. Koroga huku ikipikika hadi ianze kugeuka rangi na kuanza kuachana. Usiache mkono kuroga isije kufanya madonge. Tia hiliki na vanilla, endelea kuipika. Itakapogeuka rangi vizuri mimina katika sinia na haraka uitandaze kwa mwiko huku ukiuchovya katika maji na kuendelea kuitandaza hadi ikae sawa kote. Pitisha kisu kuikataka ili ikipoa iwe wepesi kuitoa vipande.
Kila inapozidi kupoa na kukaa ndipo fagi inakauka na kumumunyuka.
Jinsi ya kuandaa Biriani Na Sosi Ya Nyama Ya Mbuzi
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama Ya Mbuzi - 1 Kilo
Mchele - 4 Magi
Vitunguu - 3
Nyanya - 2
Nyanya kopo - 3 vijiko vya chai
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Garam Masala (mchanganyiko wa bizari) - 2 vijiko vya supu
Hiliki - 1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Mafuta - Β½ kikombe
Zaafarani au rangi za biriani za kijani na manjano/orenji
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Sosi Ya Nyama
Changanya nyama na thomu, pilipili, chumvi na nusu ya garam masala. Tia katika treya ya oveni uipike nyama (Bake) hadi iwive. Au iwivishe kwa kuichemsha. Katika kisufuria kingine, tia mafuta (bakisha kidogo ya wali) kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi, kisha tia nyanya, nyanya kopo, bizari zote nyingine zilizobakia.
Namna Ya Kupika Wali
Mchele - 4 magi
Mdalasini - 1 kijiti
Hiliki - 3 chembe
Kidonge cha supu - 1
Chumvi
Osha na roweka mchele wa basmati. Tia maji katika sufuria uweke jikoni. Tia kidonge cha supu, mdalasini, hiliki na chumvi . Yakichemka maji tia mchele, funika upike hadi nusu kiini kisha uchuje kwa kumwaga maji. Tia mafuta kidogo katika mchele na zaafarani iliyorowekwa au rangi za biriani kisha rudisha mchele katika sufuria ufunike na upike hadi uwive. Pakua wali katika sahani kisha mwagia sosi ya nyama juu yake, pambia kwa kukatika nyanya, pilipili mboga na figili mwitu (Celery) au mboga yoyote upendayo.