Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!
JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.
Mke akamwambia mumewe; "Tupige magoti tusali",
Wakapiga magotiβ¦:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emenβ¦
Updated at: 2024-05-25 18:05:38 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.
Mke akamwambia mumewe; "Tupige magoti tusali",
Wakapiga magotiβ¦:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emenβ¦
MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emenβ¦
MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimyaβ¦
MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: β¦β¦.!!
MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.
Chezea mawaifu walokole wewe!
Updated at: 2024-05-25 17:55:37 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule "Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny" anakuuliza "pckt mny" ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha "pocket money" af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Updated at: 2024-05-25 17:15:27 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu? sipendagi ujingaπΆπ» na kitu hela mm!
Wachaga kweli kiboko: Mcheki huyu mchaga na mbuzi!!!
Updated at: 2024-05-25 18:12:25 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. ππ
Updated at: 2024-05-25 17:09:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wasichana wafupi wananifurahisha sanaβ¦. Yaan siku ya Valentine, wakivaa magauni mekundu huwa wanakuwa kama Fire extinguishers au mitungi ya Oryx πππππ
Updated at: 2024-05-25 17:54:58 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwalimu aliingia darasani akiwa amechoka kinoma akawambia wanafunzi.
'leo tutajifunza kipindi cha dini " wanafunzi wakiwa wanajiandaa ili kuendelea na kipindi mwalimu akajiegesha kwenye kiti klichokua karibuu yake baada ya dakika kadhaa mwalimu alipitiwa na usingizi, ghafla alingia mkurugenzi na kusimama pembeni mwa kile kiti alichokalia mwalimu ghafla kmya kikatawala darasani kiasi cha kunfanya mwalimu ashtuke usingizini aliamka huku akipiga miayo alpotupa jicho pembeni alimuona mkurugenzi kasimama pemben! akiwa anababaika alifungua kinywa na kusema ' Hivi ndivyo walivyolala wanafunzi wa YESU walipokua wakimsubli kule mlimani, je kuna mwenye swal? mkurugeni pale alipokua akapiga makofi na kumsifia mwalimu kwa kufundisha kwa vitendo.
Je % Ngapi unampa mwalimu kwa kusolve kibarua chake.????
Updated at: 2024-05-25 17:13:37 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) Mtotoβ¦Mama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasaβ¦..