Sidebar with Floating Button
MHUBIRI
AckyShine

SALA YA BWANA: SALA YA BABA YETU

Featured Image

Baba yetu uliye mbinguni
Jina lako litukuzwe
Ufalme wako ufike
Utakalo lifanyike
Duniani kama mbinguni
Utupe leo mkate wetu wa kila siku
Utusamehe makosa yetu
Kama tunavyowasamehe
Na sisi waliotukosea
Usitutie katika kishawishi
Lakini utuopoe maovuni.
Amina.

83 Comments

SALA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU

Featured Image

Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, utulinde katika vita, uwe kinga yetu katika maovu na maoteo ya shetani, Mungu amtiishe, tunaomba sana, nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni kwa nguvu ya Mungu uwaangushe motoni shetani na pepo wabaya wengine wote, wanaozunguka duniani, ili kuzipoteza roho za watu. Amina.

88 Comments

Sala ya Usiku kabla ya kulala

Featured Image

Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.

SALA YA KUSHUKURU

Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji uliyotujalia leo. Amina.

Baba yetu …

Salamu Maria …

88 Comments

SALA YA MAPENDO

Featured Image

Mungu wangu, nakupenda zaidi ya cho chote, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina

83 Comments

Kumbuka ee Bikira Mwenye Rehema

Featured Image
83 Comments

AMRI ZA KANISA

Featured Image

1. HUDHURIA MISA TAKATIFU DOMINIKA NA SIKUKUU ZILZOAMRIWA

2. FUNGA SIKU YA JUMATANO YA MAJIVU; USILE NYAMA SIKU YA IJUMAA KUU

3. UNGAMA DHAMBI ZAKO WALAU MARA MOJA KILA MWAKA

83 Comments

Matendo ya Rozari Takatifu: Mchanganuo kwa siku zote za Saba za Juma

Featured Image
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi) Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu. Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani. Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
84 Comments

ROZARI YA MOYO MTAKATIFU WA YESU

Featured Image

Tumia tasbihi ya kawaida yenye chembe ndogo 53.

Kwenye Msalaba Sali:

“Ee Yesu tupe moyo wako kama amana ya upendo wako na kimbilio letu, ili tupate pumziko salama wakati wa maisha yetu na faraja tamu saa ya kufa kwetu”.
Baba Yetu ……..
Salamu Maria ……. (mara tatu)
Nasadiki ………..

87 Comments

SALA YA KUMWABUDU BWANA YESU KATIKA SAKRAMENTI TAKATIFU

Featured Image

Ee Yesu Kristu,/ Bwana wangu na Mungu wangu/ ambaye ninasadiki kuwa upo hapa/ katika Sakramenti Takatifu ya Altare;/ pokea kitendo hiki cha kukuangukia kifudi fudi/ kama ishara ya tamaa niliyonayo ya kukuabudu Wewe/ bila kuchoka/ na kukushukuru kwa mapendo yako makubwa/ yasiyo na kipimo/ ambayo Moyo wako Mtakatifu sana/ unawaka katika Sakramenti

83 Comments

ROZARI YA MATESO SABA YA BIKIRA MARIA

Featured Image

Tumia Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria iliyo na mafungu 7 yaani mateso 7 yenye Salamu Maria saba kwa kila teso.

TESO LA KWANZA

Mzee Simeoni aliagua kuwa Moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga.
Tuombe neema ya kuvumilia mateso.
Mama wa mateso utuombee.

84 Comments
📘 About 🔒 Login 📝 Register 📞 Contact