Sidebar with Floating Button
MHUBIRI
โ˜ฐ
AckyShine

Sababu inayopelekea kushindwa kuishi maisha ya ndoto zako

Featured Image
0 Comments

Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara

Featured Image

HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
๐Ÿ’ฅMama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.

0 Comments

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?

Featured Image

Kwa mujibu wa Biologia, baada ya tendo la kukutana kimwili takribani mbegu milioni 200 hadi 300 hutolewa na mwanaumeโ€ฆhalafu zote huanza kupiga mbizi kuogelea kwenye njia safarini kukutana na yai la kike.

Ajabu ya kwanza ni kwamba sio zote 200 - 300 ambazo hufanikiwa kulifikia yai( nyingi huchoka na kufia njiani maana si mashindano ya mchezo mchezo).
Ajabu ya pili ni kwamba kati ya hizi 300 zinazofanikiwa kufikia yai, ni moja tu..moja tu itakayoshinda nakufanikiwa kupenya na kurutubisha yai, na kwa mantiki hii ILIYOSHINDA NI WEWE HAPO.

0 Comments

Mbinu 5 za kukunufaisha maishani

Featured Image

Mbinu 5 za kukufanikisha maishani Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu fulani kufanikiwa.

0 Comments

JITAMBUE: Kipi hauna kati ya pesa na muda?

Featured Image

Watu ambao hawana pesa ila wana muda wa bwerere. Hawajui thamani ya muda. Hawa ndo wale ambao hawajui cha kufanya. Anaamka mpaka analala usiku hana specific timetable. Unaweza kumkuta anaenda dukani ukamwambia nisindikize saluni na akakubali. Yupo yupo tu. Unaweza kuta ameingia Facebook hajui hata kwa mini. Basi tu kwa sababu ana bando. Akiperuzi akaona mahali wanaongelea mpira yumo

0 Comments

Angalia jinsi maamuzi yako ya jana na ya leo yanavyoweza kukuathiri

Featured Image

Nimeitoa kwa Comrade Markus Mpangala na kuitafsiri kwa Kiswahili (kisicho rasmi sana).
Mwaka 1998 "Google" walitaka kuiuza kampuni yao kwa "Yahoo" kwa dola Milioni 1 (sawa na Shilingi Bilioni 2) lakini Yahoo wakakataa. Yani Yahoo wakakataa kuinunua Google.

0 Comments

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

Featured Image

Mwaka umefika mwisho, zimebaki siku tatu tu
kuingia mwaka mwingine lakini yapo mengi
niliyojifunza mwaka huu na pengine ningepesha
kushare:

0 Comments

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi

Featured Image

Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka.
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.

0 Comments

USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE

Featured Image

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.

Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.

0 Comments

Angalia jinsi muda wako unavyopotea

Featured Image

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.

Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?

0 Comments
๐Ÿ“˜ About ๐Ÿ”’ Login ๐Ÿ“ Register ๐Ÿ“ž Contact