Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo tunaangalia mapishi ya fish finger ( sijui kama unaweza kusema kidole cha samaki)!, Ni mlo mzuri hasa kuliwa kama kitafunio au mboga ya pembeni.
Mahitaji
500g Fileti ya samaki 120g Chenga za mkate 100g Unga wa ngano Mayai 2 Ndimu 1 Kitunguu saumu 1 Kotmiri Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Menya vitunguu saumu kisha visage
Katakata fileti kwa muundo wa mraba (kama vidole) kisha paka mchanganyiko wa vitunguu saumu
Kata ndimu na kamulia kwenye fillet yako
Weka chenga za mkate kwenye bakuli kisha uchanganye chumvi kiasi na kata kata kotmiri majani 3 na uchanganye pamoja.
Kwenye bakuli lingine weka mayai na uyapigepige yawe kama uji mzito
Weka unga kwenye bakuli jingine.
Chukua kipande cha fillet kiweke unga kidogo kisha kizamishe kwenye yai na baada ya hapo kizamishe kwenye mchanganyiko wa chenga za mkate. Fanya hivyo kwa vipande vyote.
Weka mafuta kwenye kikaago na subiri yachemke kisha weka fillet zako vizuri na zikaange pande zote hadi zimekuwa rangi ya brown ( hakikisha moto sio mkali sana).
Updated at: 2024-05-25 10:34:53 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Vikombe
Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu
Maziwa ΒΎ Kikombe
Iliki Kiasi
Mafuta ya kukarangia Kiasi
Shira
Sukari 1 Kikombe
Maji ΒΎ Kikombe
Vanila Β½ Kijiko cha chai
Zafarani (ukipenda) Kiasi
Jinsi ya kupika na kuandaa
Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine. Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo. Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi. Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha. Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote. Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:46 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji:
Unga sembe glass 1 Unga ngano glass 1 Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo) Maziwa glass 1 Mafuta 1/2 glass Mayai 4 Iliki iliosagwa 2tbs Bp 2tbs
Jinsi ya kupika:
Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe. Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.
Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.
Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi
Mchele wa basmati - 3 vikombe
Kuku - Β½
Bilingani - 2 ya kiasi
Viazi - 4
Vitunguu - 2
Kitunguu (thomu/galic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 2
Chumvi - kiasi
Garama masala (mchanganyiko wa bizari) - 1 kijiko cha chai
Hiliki ya unga - ΒΌ kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia wali - ΒΌ kikombe
Mafuta ya kukaangia viazi na bilingani - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele. Kata kuku vipande upendavyo safisha Kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu, na bizari mchanganyiko (garama masala). Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria. Menya na kata viazi kaanga weka kando. Kata kata bilingani slesi nene kaanga, chuja mafuta weka kando. Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi. Tia vipande vya kuku, ukaange kidogo. Tia supu ya kuku, mchele, tia hiliki, ufunike hadi karibu na kuwiva kabisa. Tia viazi na bilingani uchanganye kidogo, kisha tia katika oven imalizike kupikika pilau humo au unaweza kuendelea kufunika juu ya jiko hadi pilau iwive. Pakua katika sahani ikiwa tayari kuliwa kwa saladi ya mtindi.
Updated at: 2024-05-25 10:37:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 300gm
Siagi 225gm
Icing Sugar 60gm
Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) - 225gm
Vanilla β Vijiko 2 vya chai
Yai -1
Baking Powder Β½ kijiko cha chai
Njugu za vipande Β½ kikombe cha chai
Njugu zilizosagwa ΒΌ kikombe cha chai
JINSI YA KUTAYARISHA
Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike. Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k) Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350Β°C , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe Yayusha chokoleti tia kwenye bakuli ndogo. kisha paka kwa kijiko au chovyea upande mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga. Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Chenga za biskuti - 3 gilasi
Mtindi (yogurt) - 1 Kopo (750g)
Maziwa ya unga - 1 gilasi
Siagi - 10 Vijiko vya supu
Sukari - Β½ gilasi
Lozi zilizomenywa vipande vipande - Β½ gilasi
Nazi iliyokunwa - Β½ gilasi
Vanilla - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Katika mashine ya kusagia (blender), tia mtindi, sukari, siagi na vanilla na usage pamoja hadi ichanganyike. Mimina katika bakuli la kiasi. Tia vitu vilivyobakia na uchanganye vizuri. Mimina kwenye treya ya kuchomea na uvumbike katika oveni moto wa 350Β° hadi ishikamane na kuwa tayari. Iaache ipoe kisha katakata vipande na tayari kwa kuliwa.
Baada yakuwa imeshaiva, ukipenda unaweza kupakiza jamu au karameli ya tayari kwa juu, kisha ukarudisha kwenye oveni moto wa juu kidogo kwa ladha nzuri zaidi
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI VYA TUNA
Tuna (samaki/jodari) - 2 Vikopo
Vitunguu (kata kata) - 4
Nyanya zilizosagwa - 5
Nyanya kopo - 3 Vijiko vya supu
Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo - cubes) - 4
Dengu (chick peas) - 1 kikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic)&Tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Hiliki - 1/4 kijiko cha chai
Mchanganyiko wa bizari - 1 kijiko cha supu
Chumvi - kiasi
Pilipili manga - 1 Kijiko cha chai
Vipande cha Maggi (Cube) - 2
VIAMBAUPISHI VYA WALI
Mchele - 3 Vikombe vikubwa (Mugs)
Mdalasini - 2 Vijiti
Karafuu - chembe 5
Zaafarani - kiasi Jirsh (Komamanga kavu au zabibu kavu -raisins) - 1/2 Kikombe
JINSI YA KUANDAA
Kosha Mchele na roweka. Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) chuja mafuta uweke kando. Kaanga viazi, epua Punguza mafuta, kaanga nyanya. Tia thomu/tangawizi, bizari zote, vipande vya Maggi, nyanya kopo, chumvi. Mwaga maji ya tuna iwe kavu, changanyisha kwenye sosi. Tia zaafarani kidogo katika sosi na bakisha ya wali. Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu. Karibu na kuwiva, chuja maji utie katika chombo cha kupikia katika jiko (oven) Nyunyizia zaafarani, mwagia vitunguu, viazi, na dengu juu ya wali. Mwagia sosi ya tuna na pambia jirshi (au zabibu). Funika wali na upike katika jiko moto wa 450ΒΊ kwa muda wa kupikika wali. Epua upakue.