Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 2 Vikombe
Cocoa ya unga - 1 Kijiko cha supu
Sukari ya hudhurungi - 1 Kikombe
Siagi - ΒΎ Kikombe
Yai - 1
Molasses - ΒΌ Kikombe
Baking soda - 2 vijiko vya chai
Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Karafuu ya unga - Β½ kijiko cha chai
Chumvi Β½ kijiko cha chai
Vanilla Β½ kijiko cha chai
MAANDALIZI
Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando. Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti. Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili. Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri. Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike. Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri. Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.) Tengeneza viduara vidogo vidogo.
Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka
Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.
Oka katika oven 350ΒΊF kwa muda wa dakika 15.
Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi. Panga kwenye sahani tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kupata takriban gilasi 6
Mabungo - 3
Maji - 6 au 7 Gilasi
Sukari - kiasi upendacho
Chumvi - kidogo sana
Namna Ya Kutayarisha:
Kata mabungo na toa nyama yake tia katika mashine ya kusagia. Tia maji, sukari na chumvi usage kidogo tu. Chuja kisha mimina katika jagi uweke katika friji. Mimina katika gilasi.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 4 Vikombe vya chai Sukari ya laini (icing sugar) - 1 Kikombe cha chai Baking powder - 2 Vijiko vya chai Mayai - 2 Siagi au margarine - 1 Kikombe cha chai Vanilla -1 Kijiko cha chai Maziwa ya kuchanganyia - kiasi Tende iliyotolewa koko - 1 Kikombe ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe
MAANDALIZI
Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine. Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane. Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana. Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika. Vumbika (bake) moto wa 350Β°F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive. Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Blue band vijiko vikubwa 2 Maziwa vikombe 2 Royco kijiko kikubwa 1-2 Pilipili manga (unga) kijiko cha 1 Chumvi kiasi Maji lita 2-3 Boga kipande Β½ Viazi mviringo 2 Vitunguu 2 Karoti 2 Nyanya 2
Hatua
β’ Menya boga, viazi, karoti, nyanya na kwaruza weka kwenya sufuria kubwa. β’ Menya, osha na katakata vitunguu kisha ongeza kwenye mboga. β’ Ongeza maji na chumvi chemshwa mpaka vilainike. β’ Pekecha ikiwa jikoni na moto kidogo β’ Ongeza blue band, maziwa royco na pilipili manga ukikoroga kwa dakika 5. β’ Onja chumvi na pakua kama supu. Uwezekano Tumia siagi badala ya margarine.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 2 Β½ gilasi
Sukari ΒΎ gilasi
Samli 1 gilasi
Mayai 2
Baking powder 2 kijiko vya chai
Vanilla 1 Β½ kijiko cha chai
Maganda ya chungwa 1
MAPISHI
Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri. Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya. Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni. Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake. Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam. Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180Β C.
Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Mashonanguo mkono 1 Tui la nazi kikombe 1 Karanga zilizosagwa kikombe Β½ Mafuta vijiko vikubwa 4 Kitunguu 1 Nyanya ndogo 2 Chumvi kiasi
Hatua
⒠Chambua mashona nguo mateke, osha na katakata. ⒠Menya osha na katakata kitunguu. ⒠Osha, menya na katakata nyanya. ⒠Kaanga karanga, ondoa maganda na saga zilainike. ⒠Kuna nazi na chuja tui. ⒠Kanga kitunguu, weka nyanya na koroga mpaka zilainike. ⒠Weka mashona nguo na chumvi kisha koroga sawa sawa, funikiakwa dakika 5 -10. ⒠Changanya tui la nazi na karanga, ongeza kwenye hizo mboga ukikoroga kwa dakika 5, punguza moto ili ziive taratibu. ⒠Onja chumvi na pakua kama kitoweo. Uwezekano Changanya mnavu, mgagani, mashonanguo kidogo ki¬dogo au mboga nyingme. Tumia maziwa au krimu badala ya tui la nazi. Weka nyama au dagaa au samaki au mayai badala ya - karanga.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Nyanya 1Β kg Maji Iita Β½ Chumvi kijiko kidogo 1 Sukari
Hatua
β’ Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike. β’ Chuja juisi. β’ Pima juisi - vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka kwenya sufuria safi . β’ Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke. β’ Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa kunywa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi Limao 1 kubwa Kitunguu swaum Tangawizi Chumvi Pilipili
Matayarisho
Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.
Note: Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.
Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan
Updated at: 2024-05-25 10:23:16 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama ya mbuzi au ngβombe ya mafupa - 2 LB
Mchanganyiko wa dengu (hadesi, mchele, chooko, ngano, dengu n.k au nunua ya tayari iliyokwisha changanywa - 2 Vikombe
Kitungu maji (vikate vidogo) - 1
Mafuta - ΒΌ Kikombe
Nyana kata ndogo ndogo - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawazi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu
Bizari ya haliym - 2 vijiko vya supu
Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha nyama na chumvi Β½ kijiko mpaka iive, toa mafupa. Chemsha mchanganyiko wa dengu mpaka ziive. Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu vilainike, tia thomu na tangawizi, bizari ya haliym, nyanya ya kopo. Kaanga mpaka iwive. Tia nyama iliyowiva na supu yake kidogo. Tia mchanganyiko wa dengu tia kwenye mashine ya kusaga (blender), saga na ile supu ya nyama isagike vizuri Mimina kwenye sufuria changanya, tia ndimu kidogo, acha moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 15. Tia katika bakuli, pambia kwa vitunguu vilivyokaangwa vya rangi ya hudhurungi vikavu, pilipili mbichi (ukipenda) na kotmiri, ikiwa kuliwa.