Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes
Updated at: 2024-05-25 10:23:08 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 4 Vikombe
Sukari - 1 Kikombe
Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi - 454 gms
Mayai - 2
Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) - 1 Kikombe
Vanilla - 2 Vijiko vya chai
Cornflakes - Β½ kikombe
JINSI YA KUANDAA
Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy) Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy) Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko. Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed) Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375Β°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) 100g Sukari (sugar) 100g Siagi isiyokuwa na chumvi (unsalted butter) 100g Mayai (eggs) 2 Vanila 1 kijiko cha chai Chumvi pinch Warm water 3 vijiko vya chakula
Matayarisho
Kwanza washa oven moto wa 200Β C. Baada ya hapo saga butter na sukari mpaka viwe laini kisha tia mayai na uendelee kusaga mpaka vichanganyike vizuri kisha tia unga, vanila, chumvi na na maji na usage mpaka upate uji usiokuwa mzito sana au mwepesi sana. Baada ya hapo utie kwenye baking tin na u bake kwa muda wa dakika 25 na mpaka cake yako iive yani juu na chini iwe ya brown na ukidumbukiza kijiti katikati kinatoka kikiwa clean. Baada ya hapo itoe kwenye tin na uiache ipoe. Ikisha poa itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mackerel 2 Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2 Limao (lemon) 1/2 Chumvi (salt) kiasi Curry powder 1/2 kijiko cha chai Coriander powder 1/2 kijiko cha chai Mafuta 1 kijiko cha chai
Matayarisho
Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.
Updated at: 2024-05-25 10:34:44 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
β’ Maziwa ya mama pekee ndio chakula na kinywaji cha mtoto bora zaidi kwa watoto kwa miezi sita ya kwanza. β’ Ni jambo la muhimu sana kunyonyesha watoto wachanga kwa muda wa miezi minne na uendelee kunyonyesha hadi mtoto atakapofikisha mwaka mmoja na kuendelea.
β’ Mtoto akifikisha miezi sita ndio wakati muafaka wa kumpa vyakula vya nyongeza vilivyotayarishwakatika hali ya usafi.
β’ Onana na mnasihi akushauri kuhusu muda na jinsi ya kumuanzishia mtoto wako vyakula vya nyongeza
β’ Vyakula vya ngogeza viwe ni vya mchanganyiko wa makundi yafuatayo ya chakula:- vyakula vya nafaka, venye asili ya nyama, mbogamboga na matunda, mafuta na sukari (kiasi). Lisha kila chakula kwa siku kadhaa kwa kufuatanisha kabla hujaaza chakula chengine kipya.
β’ Usimuachilie mtoto alale kama chupa ya maziwa ingali mdomoni, ili kuepukana na kuoza kwa meno na madhara ya.
β’ Watoto wanaopewa maziwa ya mama pekee hawaugui mara kwa mara, na wakiugua, makali ya ugonjwa hupungua na hupona mapema kwa sababu yale maziwa ya mwanzo ya njano yenye viini vingi vya kumkinga dhidi ya magonjwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:37 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Boga la kiasi - nusu yake
Tui zito la nazi 1 Β½ gilasi
Sukari Β½ kikombe
Hiliki Β½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi. Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi. Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika. Epua mimina katika chombo likiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 6 Vikombe
Sukari ya kusaga 2 vikombe
Siagi 500 gm
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Kastadi Β½kikombe
MAPISHI
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli. Tia unga na baking powder na Kastadi. Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray). Pika (bake) katika oven moto wa 350Β° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Bizari ya unga (cummin powder) - 1 Kijiko cha chai
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Safisha daal kwa kutoa mawe ikiwa yapo, kisha osha na roweka dakika 15 hivi. Kisha chemsha kwa kutia maji, bizari ya manjano, chumvi, pili pili ya unga na maji ya ndimu hadi iive na kuvurujika. Halafu chukua kisufuria na kaanga kitungu, kisha thomu na mwisho tia bizari ya pilau. Kisha mimina mchanganyiko wa kitunguu kwenye sufuria ya daal (iliyokwisha iiva)na uchanganye na iwache motoni kidogo itokote. Ukipenda mimina mchanganyiko kwenye blenda na usage mpaka iwe laini. Tia kwenye bakuli na itakuwa tayari kuliwa na wali na samaki ukipenda
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tango 1/2 Kitunguu 1/2 Cherry tomato 8 Lettice kiasi Green olives kidogo Black olives kidogo Hoho jekundu 1 Carrot Giligilani kidogo
Salad dressing Yogurt 1/2 kikombe Swaum 1/2 kijiko cha chai Limao 1/2 Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai Chumvi kidogo Olive oil kiasi
Matayarisho
Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.
Jinsi ya kupika Pilau ya Mpunga Na Nyama Ya Ngβombe
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mpunga - 4 vikombe
Nyama - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 3
Mbatata/viazi - 7 vidogodogo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu
Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 3 vipande
Hiliki - 7 punje
Pilipili manga nzima - 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Mafuta - Β½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele weka kando Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo. Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga. Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi. Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata. Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari. Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.
Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga
Updated at: 2024-05-25 10:23:16 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama isiyokuwa na mifupa - 1 Β½ Lb(ratili) Mchele wa Basmati (rowanisha) - 3 Magi Vitunguu maji - 2 Mchanganyiko wa mboga za barafu - 1 Magi (karoti, mahindi, njegere) Pilipili Mbichi - 3 Pilipili mboga kijani na nyekundu - 1 Pilipili manga - Β½ kijiko cha chai Chumvi - Kiasi Sosi ya soya (soy sauce) - 5 Vijiko vya supu Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu Mchanganyiko wa bizari (garam masala) - 1 Kijiko cha supu Kotmiri iliyokatwa - Β½ Kikombe Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutaarisha
Ndani ya sufuria, tia mafuta yakipata moto kaanga vitunguu mpaka ziwe rangi ya hudhurungi. Kisha tia nyama iliyokatwa vipande vidogo vidogo pamoja na maji ya kiasi na viungo vyote isipokuwa mchele, mboga zote na kotmiri. chemsha mpaka nyama iwive na maji yakauke. Halafu changanya na mboga na iwache kwa muda wa dakika kumi kisha tia kotmiri na umimine kwenye bakuli au treya ya oveni na uweke kando. Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja, kisha umwagie juu ya ile treya ya nyama. Nyunyizia mafuta na sosi ya soya na ipike katika oveni moto wa 350Β° kwa muda wa dakika 20 hivi. Ukishawiva, uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa