Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Unganisha imani na maisha yako kupitia π Sala, π Masomo ya Misa, π Mafundisho, π‘ Tafakari, π° Makala, na π My System kwa usimamizi wa maisha binafsi. Tunakukaribisha kwenye safari ya kiroho na kimwili!.
Mapishi ya wali mtamu Wa Nazi Kwa Maharage Na Samaki Nguru Wa Kukaanga
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Wali:
Mchele mpunga - 4 Vikombe
Tui la nazi - 6 vikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele weka kando. Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi. Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.
Maharage Ya Nazi
Maharage - 3 vikombe
Tui la nazi zito - 1 kikombe
Tui la nazi jepesi - 1 kikombe
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa -1 kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha maharage mpaka yaive. Katiakatia kitunguu maji na tia thomu, tia na tui jepesi kikombe kimoja. Tia tui zito endelea kuweka katika moto mdogomdogo hadi yakaribie kukauka yakiwa tayari.
Samaki Nguru Wa Kukaanga
Samaki Wa Nguru - 4 vipande
Kitunguu saumu(thomu/galic) & tangawizi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi - 4
Ndimu - 2 kamua
Bizari ya samaki -1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Mwoshe samaki kisha mtie kitunguu thomu, tangawizi ilosagwa, chumvi, pilipilimbichi ilosagwa, ndimu na bizari ya samaki. Mwache akolee viungo kwa muda kidogo. Makaange katika mafuta hadi aive akiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 1 Kikombe
Sukari ya kusaga - 3/4 Kikombe
Siagi - 125 gms
Yai - 1
Baking powder - 1/2 kijiko cha chai
Zabibu kavu - 1/2 kikombe
Cornflakes iliyovunjwa (crushed) - 2 Vikombe
Vanilla - 1 kijiko cha chai
MAANDALIZI
Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri. Tia baking powder, zabibu na unga na changanya vizuri. Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni. Tengeneza viduara vidogo vidogo. Weka cornflakes katika sahani ya chali (flat) na zungusha viduara humo kisha upange katika sinia ya oveni. Pika katika moto wa 350ΒΊF kwa muda wa dakika 20-25 hadi vigeuke rangi na viwive.
Mapishi ya Muhogo Na Mbatata Za Nazi Kwa Nyama Ngombe
Updated at: 2024-05-25 10:37:34 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo - Mahitaji Ya Nyama
Nyama ya nβgombe ya mifupa - 3Β lb
Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu
Kitunguu thomu - 1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau/jira/uzile (cumin) - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) - 1 cha wastan
Pilipili mbichi - 3 Zilizosagwa
Chumvi - Kiasi
Vipimo - Muhogo Na Mbatata/Viazi
Muhogo menya na ukate vipande pande - 2
Mbatata/Viazi menya ukate vipande vikubwa kiasi - 5 kiasi
Tui la nazi zito - 1 gilasi
Nyanya ilokatwakatwa au kusagwa - 1
Kitunguu kilokatwakatwa (chopped) - 1 kiasi
Bizari ya mchuzi - kiasi
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha nyama kisha weka katika pressure cooker au sufuria. Tia viungo vyote vya nyama uchanganye vizuri, kisha ikorogekoroge mpaka maji yake yakaribie kukauka. Usifunike. Tia maji kiasi ya kuivisha nyama na kubakisha supu yake kiasi ya kuivisha muhogo na mbatata. Muda wa kuivisha nyama inategemea nyama yenyewe na kama unatumia pressure cooker ni takriban dakika 35-40. Ikiwa sufuria ya kawaida utakuwa unaikoroga. Mimina ndani ya supu, muhogo, mbatata, nyanya, kitunguu, bizari ya mchuzi, chumvi. Acha ichemke uive muhogo na viazi. Tia tui la nazi, changanya vizuri acha kwenye moto dakika chache tu. Epua ikiwa tayari. Tolea na achari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama (kata vipande vidogodogo) - Β½ kilo
Maharage - 3 vikombe
Mahindi - 2 vikombe
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kabichi lililokatwa - 2 vikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Vidonge vya supu - 2
Chumvi - kiasi
Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula
Namna Yakutayarisha
Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi. Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi. Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi. Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi. Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive. Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Dagaa (dried anchovies packet 1) Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo) Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2) Kitunguu maji (onion 1) Limao (lemon 1/4) Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop) Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai) Mafuta (vegetable oil) Hoho (green pepper)
Matayarisho
Chambua dagaa kwa kutoa vichwa vyao na utumbo, baada ya hapo waloeke katkika maji ya moto kwa muda wa dakika 5 na uaoshe tena katika maji ya baridi na uwakaushe uwaweke pembeni. Ukishamaliza katakata kitunguu na uandae nyanya tayari kwa upishi. Bandika sufuria ya kupikia dagaa jikoni na utie mafuta, yakishapata moto tia vitunguu pamoja na dagaa. Kaanga mpaka dagaa wawe light brown kisha tia nyanya, chumvi na pilipili. Pika nyanya mpaka ziive (ukitaka kujua kama nyanya zimeiva utaona zinatengana na mafuta) Baada ya hapo kamulia limao kidogo sana na tia pilipili hoho na zipike kama dakika mbili. kisha ipua. Ukisha maliza kupika dagaa andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi Limao 1 kubwa Kitunguu swaum Tangawizi Chumvi Pilipili
Matayarisho
Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.
Note: Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.
Jinsi ya kupika Pilau ya Nyama ya Kusaga Na Mboga Mchanganyiko
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 2 Mugs
Viazi - 3
Nyama ya Kusaga - 1 Pound
Mboga mchanganyiko za barafu - 1 Mug
(Frozen vegetable)
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 2 vijiko vya supu
Garam masala - 1 kijiko cha supu
Nyanya - 1
Kitungu maji - 1
Mdalasini nzima - 1 vijiti
Karafuu - 3 chembe
Pilipili mbichi - 1
Chumvi - kiasi
Maji - 2 Β½ Mugs
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele na uroweke kiasi kutegemea aina ya mchele. Katakata viazi kaanga katika mafuta, toa weka kando. Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown). Tia nyama ya kusaga, thomu na tangawizi, pilipili, bizari zote na chumvi. Kaanga hadi nyama iwive. Katakata nyanya uliyokatakata itie katika mchanganyiko wa nyama na endelea kukaanga kidogo tu. Tia mboga ya barafu (frozen vegetables) Tia maji, kidonge cha supu. Yatakapochemka tia mchele. Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa Β½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:06 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 4 Vikombe vya chai
Siagi - 1 Kikombe cha chai
Hiliki Β½ Kijiko cha chai
VIAMBAUPISHI:SHIRA
Sukari - 2 Vikombe vya chai
Maji - 1 Kikombe cha chai
Vanilla Β½ Kijiko cha chai
(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.
JINSI YA KUTENGENEZA
Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki. Changanya vizuri isiwe na madonge. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. . Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.
Jinsi ya kutengeneza Cookies Za Tende Na Tangawizi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe vikombe 4
Baking soda 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi 400 gms
Sukari Β½ kikombe
Tende chambua ukatekate ifikie ΒΎ kikombe
Tangawizi ya unga vijiko 2 vya chai
Vanilla 1 kijiko cha chai
Yai 1
Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia.
MAANDALIZI
Changanya siagi na sukari katika mashine usage mpaka iwe laini nyororo. Tia yai uchanganye vizuri Tia tende na vanilla, tangawizi uchanganye vizuri. changanya unga na baking soda kisha, mimina kidogo kidogo huku unachanganya kwa kijiko cha ubao (mwiko). Unga ukiwa mzito ongeza vijiko 2 vya maziwa. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi kisha uchome (bake) katika over moto mdogo wa kiasi dakika 15 vigeuke rangi viwive. Epua vikiwa tayari